Kuhusu Mbunifu Blog
Matokeo ya tafiti mbalimbali yanaonesha kuwa vijana wengi wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu wanakabiliwa na changamoto ya ajira.
Zipo pia tafiti zinazoonesha kuwa vijana na watu wazima walio katika ajira mbalimbali, wakiwemo wajasiriamali, wanakabiliwa na changamoto ya ufahamu mdogo wa stadi za maisha ya kawaida, za ujasiriamali, na ubunifu.
Kutokana na ukweli huu, kuna ushauri kutoka kwa wadau wa masuala ya elimu, kwamba, juhudi zinatakiwa kufanywa kuwapatia vijana na watu wazima stadi hizi.
Kupitia ushauri huu, pamoja na maarifa na uzoefu wa ujasiriamali na ubunifu nilionao, nimepata hamasa ya kuandika makala na kuwapatia wadau hawa ili wasome, wapate maarifa haya, na wayatumie kupata mafanikio katika maisha yao.
Kwa kuzingatia hayo, blog yangu ya Mbunifu Blog itajikita katika kutoa stadi za ujasiriamali, ubunifu na uvumbuzi, pamoja na stadi za maisha kwa ujumla.
Ninaamini maarifa haya yatasaidia kuamsha bongo za wasomaji wangu na kuwafanya wachukue hatua katika kubuni, kuanzisha, kuboresha na kuongeza thamani ya shughuli au biashara zao.
Mawasiliano:
Laurent Fungavyema
- Mobile: 0785943285
- Mobile: 0718219530 (wasap)
- E-mail: Nzyy2001@gmail.com
- Instagram: @laurentfungavyema
- Facebook: Laurent Fungavyema